1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miroslav Klose, mchezaji soka wa Ujerumani

Deo Kaji Makomba
9 Juni 2020

Miroslav Klose mara chache alifanya mambo kwa njia rahisi lakini ilikuwa ni malipo kwa kutokana na juhudi zake na moja ya taaluma ya ajabu katika mchezo wa mpira duniani.

https://p.dw.com/p/3dY5q
Fußball WM Finale Argentinien Deutschland
Picha: AFP/Getty Images

Mshindi wa kombe la dunia na rekodi ya mashindano ya wakati wote ya magoli 16, mshambuliaji huyo mzaliwa wa Poland alikuwa mmoja wa washambuliaji hodari wa kizazi chake, hashikiki katika anga la soka lakini alikuwa sawa na mpira katika miguu yake ndani ya sanduku.

Hata hivyo kwa ukaribu hakufanya hivyo katika taaluma yake ya michezo na alikuwa ni mtu wa pekee katika kikosi cha Ujerumani kilichotwaa ubingwa wa kombe la dunia mwaka 2014 ambaye hakupitia katika mfumo wa soka la vijana nchini Ujerumani.

Mtoto ambaye wazazi wake walikuwa na asili ya Poland na Kijerumani ambao waliwasili nchini Ujerumani mnamo mwaka 1985, Klose alicheza soka la ridhaa katika klabu mbalimbali za kikanda wakati akijifunza ufundi seremala.

Mwishowe aliondolewa kutoka katika kucheza soka la ridhaa na kupata mafaniko yake katika ligi kuu ya kandanda ya Bundesliga akiwa na klabu ya Kaiserslautern mnamo mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 22.

Bundesliga Saison 2006/2007 Werder Bremen Clemens Fritz
Miroslav Klose, Clemens Fritz na Torsten Frings wa Werder Bremen wakishangilia bao katika mechi yao na VfL Bochum (14.10.2006)Picha: picture-alliance/Pressefoto Ulmer/B. Hake

Alikwenda kuwa na mafanikio katika ligi ya Bundesliga ambayo pia ilijumuisha nyongeza ya maendeleo yake akiwa na klabu ya Werder Bremen mnamo mwaka 2004 hadi 2007 na klabu ya Bayern Munich mnamo mwaka 2007 hadi mwaka 2011 akicheza michezo 307 na kufunga magoli 121 wakati huo pia akishinda taji la Bundesliga.

Uwezo wake wa kusubiri na kukamilisha mipira ya juu kwa hali ya kusisimua na kufurahisha kulimuwezesha kupata fursa ya kucheza mechi ya kwanza katika timu ya taifa mwaka 2001, huku hisia zake na kupenda mchezo wa haki kulimpa heshima katika maeneo mengi.

"Siwezi kufikiria mtu mwenye kazi yangu siku hizi," alisema Klose baada ya kustaafu kwake mnamo mwaka 2016. "Kwa sasa kuna waibua vipaji wengi, hivyo sifikirii kwamba kweli wachezaji wenye vipaji wanaweza kupotea bila kuonekana na kupewa fursa."
Klose ambaye kwa hivi sasa ni kocha msaidizi wa klabu ya soka ya Bayern, alimalizia muda wake wa kucheza soka kwa kipindi cha miaka mitano akiwa na klabu ya Lazio ya nchini Italia kati ya mwaka 2011 hadi mwaka 2016. Ufungaji wa magoli tele katika kila klabu, mafanikio yake makubwa yalikuja na timu ya taifa ya Ujerumani ambapo yeye ameweka rekodi ya ufungaji wa magoli mengi kwa kupachika jumla ya magoli 71 katika mechi 137 alizoichezea timu hiyo.

"Nitaendelea kucheza ilimradi naweza kuubeba mwili wangu uwanjani," Klose, wakati ule akiwa na umri wa miaka 32, alisema baada ya Ujerumani kumaliza katika nafasi ya tatu kwa mara ya pili mfululizo katika mashindano ya kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, huku muda ukiyoyoma kuelekea kustaafu.

Mshambuliaji huyo mtulivu asiyependa kuzungumza sana kwa mara nyingine tena alikuwa amekosa taji kubwa la kimataifa, baada pia kupoteza katika fainali ya kombe la dunia mwaka 2002 na wakamaliza katika nafasi ya pili katika mashindano ya kuwania kombe la Euro mwaka 2008.
Hata hivyo, aliamua kujaribu tena kwa mara nyingine, kuweka maono yake kuwa sehemu ya timu ya mwaka 2014 ya kombe la dunia nchini Brazil.

Bildergalerie berühmte Sportler und ihre Kinder
Miroslav Klose na watoto wake wavulana baada ya ushindi wa bao 1-0 katika fainali dhidi ya Argentina (Julai 13.2014)Picha: picture alliance/AP Photo/N. Pisarenko

Klose alihama kutoka Bayern kuelekea Lazio ili kupata muda wa kucheza mara kwa mara na uamuzi huo ulitoa matokeo mazuri.

Alifunga goli lake la 71 na la mwisho kwa Ujerumani katika ushindi mnono wa kihistoria wa mabao 7-1 dhidi ya wenyeji Brazil katika mechi ya nusu fainali ya kombe la dunia na kumpita Mbrazil Ronaldo aliyekuwa mfungaji bora katika mashindano ya kombe la dunia.

Siku chache baadaye alifanikiwa kutimiza ndoto yake na kuliinua kombe la dunia katika anga la Rio de Janeiro katika moja ya mchezo ambao hautasahaulika na kumvalisha taji mojawapo ya wachezaji mahiri wa soka ambaye alikaribia kukosa taji.

Deo Kaji Makomba/Reuters