1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri, Ethiopia zaanza tena mazungumzo ujenzi wa bwawa

28 Agosti 2023

Misri imesema wameanzisha tena mazungumzo kuhusiana na bwawa lenye utata nchini Ethiopia, baada ya kukubaliana mwezi uliopita kufikiwe makubaliano kufuatia mvutano wa muda mrefu ya kati ya mataifa hayo mawili.

https://p.dw.com/p/4VefN
Äthiopien Renaissance-Staudamm
Picha: Minasse Wondimu Hailu/AA/picture alliance

Kutokana na mzozo huo wa miaka mingi kuhusiana na suala hilo, Rais Abdel Fattah al-Sissi wa Misri na Waziri Mkuu Abiy Ahmed wa Ethiopa walikubaliana mwezi Julai kuhitimisha makubaliano hayo katika kipindi cha miezi minne.

Wizara ya Rasilimali za Maji na Umwagiliaji ya Misri imesema kwenye tangazo lake kwamba awamu mpya ya mazungumzo juu ya bwawa hilo la Renaissance yamianza siku ya Jumapili (Agosti 27) mjini Cairo na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka Misri, Sudan na Ethiopia.

Soma zaidi: Ethiopia, Misri, Sudan zakubali kuahirishwa ujazaji wa bwawa la Nile
Misri yapeleka mzozo wake na Ethiopia baraza la Usalama

Mradi wa bwawa hilo kubwa la Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD) wenye thamani ya dola bilioni 4.2 za Kimarekani umekuwa kitovu cha mzozo wa kikanda tangu Ethiopia ilipouanzisha mwaka 2011.

Misri inahofu ujenzi wa bwawa hilo utapunguza mgawo wake wa maji kwenye Mto Nile.