1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri na Jordan zataka Isreal itekeleze azimio la UN

12 Juni 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry na mwenzake wa Jordan Ayman Safadi wametoa himizo kwa Israel kulitii Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika azimio la mpango wa kumaliza vita huko Gaza.

https://p.dw.com/p/4gvwZ
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Ayman Safadi wakiwa katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Ayman Safadi wakiwa katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.Picha: Alaa Al-Sukhni/REUTERS

Wakizungumza katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari nchini Jordan, Safadi alisema kuaminiwa kwa sheria za kimataifa kunaweza kuwa hatarini iwapo Israel itakata kutii azimio hilo. Kadhalika Waziri Shoukry amesema kuwa azimio la Baraza la Usalama ni "lazima na kupaswa kuheshimiwa".Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu liliunga mkono pendekezo lililoainishwa na Rais wa Marekani Joe Biden la kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza.