1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WMO: Mwaka 2023 ulikuwa na ukame zaidi

7 Oktoba 2024

Shirika la Hali ya Hewa la Umoja wa Mataifa, WMO limeripoti kuwa mwaka 2023 ulikuwa ni mkame zaidi katika zaidi ya miongo mitatu kwenye mito kote ulimwenguni,

https://p.dw.com/p/4lVVD
Africa, Lesotho, Mapromoko ya Maletsunyane
Maji yakimwagika katika mmoja ya mito nchini Lesotho ambayo kulingana na Umoja wa Mataifa ilikauka mnamo mwaka 2023Picha: Cem Yücetas/Zoonar/picture alliance

Shirika hilo limesema, theluji iliyopeleka maji kwenye mito mbalimbali pia imeathirika pakubwa katika miongo mitano iliyopita, hali inayotahadharisha kwamba kuyeyuka kwa barafu hiyo kunaweza kutishia kukosekana kwa usalama wa maji kwa mamilioni ya watu ulimwenguni.

Aidha kumeshuhudiwa kupungua kwa mtiririko wa maji na kuchangia ongezeko la nyakati za ukame katika baadhi ya maeneo.

Katibu Mkuu wa WMO, Celeste Saulo amesema walipozindua ripoti hiyo hii leo kwamba ongezeko la joto kwa kiasi limechangia mabadiliko kwenye mzunguko wa kuzalisha maji, na hivyo kuzalisha maji kidogo au mengi.

Limesema, likiangazia takwimu za Umoja wa Mataifa kwamba zaidi ya watu bilioni 3.6 wanakabiliwa na upungufu wa maji kwa kama mwezi mmoja kwa mwaka, na idadi hiyo huenda ikapanda hadi milioni 5 ifikapo mwaka 2050.