1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjerumani aliyetekwa nyara Nigeria wiki mbili zilizopita ameachiwa

19 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDKJ

Mjerumani aliyetekwa nyara wiki mbili zilizopita nchini Nigeria ameachiwa huru.Mjerumani huyo aliyekua akifanya kazi za kuchimba mafuta,amekabidhiwa maafisa wa serikali katika mji wa kusini wa Nigeriá Port Harcourt.Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa..Mtumishi huyo wa kampuni la mafuta la Bilfinger na Berger alitekwa nyara agosti tatu iliyopita .Waliomteka nyara walikua wakidai kuachiwa huru wafungwa.Raia mwengine wa Ujerumani angali bado anashikiliwa mateka katika eneo tajiri kwa mafuta la Delta nchini Nigeria.Watekaji nyara wanadai wakaazi wa eneo hilo nao pia wafaidike na tija ya mafuta yao inayoyaendeya mashirika ya kimataifa.