Mjumbe wa UN Syria awasihi wafadhili wasisitishe misaada
10 Septemba 2023Matangazo
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Damascus, Pedersen amesema hali ya uchumi ndani ya Syria imezidi kuwa mbaya kuliko wakati mzozo ulipokuwa umepamba moto nchini humo.
Soma pia: UN yasema imeafikiana na Syria kuhusu uingizaji misaada
Itakumbukwa kuwa, Rais wa taifa hilo, Bashar al Assad, aliongeza kiwango sha mishahara mara mbili kwa wafanyakazi wa sekta ya umma na pensheni mwezi uliopita, hali iliyoongeza mfumuko wa bei na kuchochea maandamano yanayoendelea ambayo yalitikisa mikoa ya Sweida na karibu na mji wa Dara.
Kutokana na hali ngumu ya uchumi raia wenye hasira, walitaka Assad ajiuzulu, wito sawa na wa mwaka 2011 uliosababisha maandamano yaliyogeuka kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimeingia katika mwaka wa 13 sasa.