Mkataba mkubwa wa reli wasainiwa kati ya China na Tanzania
8 Januari 2021Makataba huo kati ya Tanzania na China unahusu ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mwanza hadi Isaka kaskazini magharibi mwa taifa hilo la afrika ya mashariki wenye urefu wa kilimota 341,unaokwenda kuanza ujenzi wa kipande cha pili cha ujenzi wa Reli hiyo inayoanzia Jijini Dar es Salaam mpaka Mwanza huku ukiwa umegawanywa kwenye vipande vitano,vya Dar es Salaam-Morogoro ambacho kimekamilika kwa asilimia 90, Morogoro –Makotopola,Makotopola-Tabora,Tabora Isaka na Mwanza Isaka,ambapo Rais Magufuli anatumia Ziara hiyo kuomba ubia zaidi na china
Tanzania ni miongoni mwa mataifa duniani ambayo yamekuwa yakibeba mzigo wa madeni kutoka China kwa muda mrefu,masharti ambayo yamekuwa yakitajwa kuwa ni magumu kwa nchi Masikini.
soma zaidi: Magufuli azindua reli ya kiwango cha kimataifa
Rais Magufuli ametumia ziara hii ya kutiliana saini kataba wa ujenzi wa reli kuiomba China kusamehe madeni wanayoidai Tanzania, la milioni 15.7 walilolibeba wakati wakijenga reli ya TAZARA ,deni la nyumba za askari takribani dola milioni 137 huku tayari Tanzania wakiwa wamelipa takribani dola milioni 67 na deni la kiwanda cha urafiki la dola milioni 15.
Mbali na kutiliana saini mkataba wa ujenzi huo wa reli ya kisasa ,Rais Magufuli imeiomba China kufikiria kuingia mkataba mwingine wa kumalizia maeneo ya ujenzi wa reli ya kisasa.
Biashara kati ya China na Afrika inatajwa kuongezeka kwa asilimia 700
Wakati huo huo mataifa hayo mawili yametanua wigo wa ubia wa kibiashara kwa kuingia makubaliano ya kutanua biashara ya Samaki kati ya Tanzania na China kama mjumbe wa baraza la taifa na waziri wa mambo ya nje wa jamhuri ya watu wa China Wang Yi anavyosema
Biashara kati ya China na Afrika inatajwa kuongezeka kwa asilimia 700 tangu miaka ya 90 huku China ikiiona Afrika kama mbia wake mkuu wa kibiashara huku ushirika wake na mataifa ya Afrika ukionekana kupiku ule wa kati ya Ulaya,Marekani na Afrika.
Mataifa mbalimbali barani Afrika yamekuwa yakijiondoa kwa kasi kwenye mfumo wa uchumi wa utawala wa kimagharibi na kuchagua mwelekeo wa China katika miaka ya hivi Karibuni ambapo biashara kati ya China na Afrika katika muongo mmoja uliopita ilipanda kutoka dola za Marekani bilioni 6.3 kwa mwaka 1999 mpaka dola bilioni 128.5 kwa mwaka 2010.
Mweleko huu mpya wa Afrika na China mbali na kungwa mkono pia umekuwa ukiibua mjadala juu ya safari ya ubia wa Afrika na China.
Mwnadishi: Dotto Bulendu DW.