1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkataba Mpya wa Kudhibiti silaha wakwamishwa

Admin.WagnerD29 Julai 2012

Mkutano unaojadili rasimu ya mkataba mpya wa kudhibiti silaha uliokwisha Ijumaa umeshindwa kufikia maamuzi juu ya mambo muhimu kuhusiana na biashara hiyo ya mabilioni ya dola.

https://p.dw.com/p/15fHI
Silaha hizi za nini lakini?
Silaha hizi za nini lakini?Picha: picture-alliance/dpa

Wakiwa mjini New York, kwa mwezi mmoja sasa washiriki wa mkutano huo walionekana wakisitasita juu ya orodha ya silaha hizo zitakazojumuishwa katika mkataba huo, unaolenga kuepusha umiliki ovyo wa silaha za kivita, ambazo aghalabu hupoteza maisha ya watu wengi katika nchi zenye mapigano.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ameeleza masikitiko yake kutokana na maendeleo hafifu ya mkutano huo, uliofikia tamati Ijumaa.

Watengenezaji wakubwa wa silaha hizo yaani nchi Ulaya, Marekani, Urusi na China na mataifa yalionekana kupinga uundwaji wa mkataba huo mpya kama vile Syria, Korea Kaskazini, Iran, Cuba, Misri na Algeria yanashiriki katika mkutano huo.

Machafuko kama haya yanaua wengi wasio na hatia.
Machafuko kama haya yanaua wengi wasio na hatia.Picha: AP

Wengi wanaupinga mkataba huu...Kwa nini lakini?

Mwezi Oktoba mwaka 2006, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura na kuamua kuwepo na mkataba utakaosimamia biashara hii ya shilaha inayokua kwa kasi, ambayo sasa ina thamani ya takriban dola bilioni 60, ambapo Marekani ilipiga kura ya" Hapana".

Serikali ya Obama ilibatilisha msimamo wa utawala wa Rais aliyemtangulia, George W. Bush, na kuliunga mkono azimio la baraza hilo la kufanya mikutano minne ya maandalizi pamoja na mkutano wa Umoja wa Mataifa kwa muda wa wiki nne mwaka huu, mahsusi kwa ajili ya kuandika rasimu ya mkataba wa biashara ya silaha.

Hatahivyo, Ban alielezea matumaini yake kuwa mkataba huo ungepitishwa kisheria na kukidhi haja iliyopo, lakini haikuwa hivyo.

Wapatanishi wamekuwa wakijaribu kuja na rasimu itakayokidhi wanasheria wa mkataba huo mzito ambao una kanuni ngumu.

Nakala za rasimu hiyo zilizosambazwa Jumanne inasema malengo ya mkataba huo ni kuweka viwango vya kusimamia biashara hiyo ya kimataifa katika silaha haramu na kuepusha na kupunguza biashara hiyo yenye athari mbaya kwa umma.

Ban Ki-moon: Nasikitika sana kusuasua huku.
Ban Ki-moon: Nasikitika sana kusuasua huku.Picha: DW

Aidha, wananaopigania mkataba huo nyeti wanasema orodha ya silaha hizo haramu ni finyu sana na inahitaji kuongezwa. Wanataka pia mkataba huo useme waziwazi kuwa silaha hizo haramu si tu za kupeleka nje ya nchi husika, bali aina zote za usafirishaji wa silaha.

Rasimu ya pili ya Argentina ni bora zaidi

Kwa mujibu wa Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International, rasimu ya pili iliyowasilishwa na Mwanadiplomasia kutoka Argentina, Roberto Moritan, ambaye ndiye aliyeongoza majadiliano hayo, ina maboresho mazuri.

Iwapo washiriki hao wat´ngefikia muafaka, Moritan angeiwasilisha rasimu hiyo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na hatimaye zingehitajika nchi 65 kuutia saini ili kuupa uwezo wa kuanza kutumika.

Mwandishi: Ndovie, Pendo Paul\AFP

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman