Mke wa Besigye asema mashitaka ya mumewe ni "uzushi"
17 Januari 2025Matangazo
Mke wa mgombea wa zamani wa urais nchini Uganda Kizza Besigye Winnie Byanyima ameyaita mashitaka dhidi ya mumewe kuwa ya "uzushi", wakati akikabiliwa na mashtaka kwenye mahakama ya kijeshimjini Kampala.
Byanyima ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la misaada, UNAIDS ameandika kwenye mtandao wa X kwamba hatarajii haki kutolewa kwa kuwa mahakama hiyo ya kijeshi ingali chini ya Rais Yoweri Museveni na mtoto wake anayelisimamia jeshi.Besigye kubakia korokoroni hadi mwaka ujao
Kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa mwezi Novemba, Umoja wa Mataifa na mashirika kadhaa ya haki za binadamu yalielezea wasiwasi kuhusu kukandamizwa kwa upinzani nchini Uganda, katikati ya ishara kwamba, kabla ya uchaguzi wa rais mwaka 2026.