Mkufunzi Löw akitaja kikosi dhidi ya Uholanzi
9 Novemba 2012Adler alikuwa kipa wa kwanza katika mechi za kombe la dunia mwaka wa 2010 nchini Afrika kusini kabla ya jeraha la mbavu kumwondoa katika dimba hilo na kumpa nafasi Manuel Neuer wa Bayern Munich, nafasi ambayo ameishikilia hadi wa leo.
Mlinda lango mwenye kipaji Marc-Andre ter Stegen hajajumuishwa lakini kocha wa Ujerumani Joachim Loew amesema yeye pamoja na Ron-Robert Zieler bado ni sehemu ya kikosi chake. Timu ya Ujerumani itakuwa bila huduma za beki wa katikati Holger Badstuber na kiungo Sami Khedira, ambao wote wana majeraha.
Kwingineko, Mwenyekiti wa klabu ya Bayern Munich Karl-Heinze Rummenige amesema klabu hiyo haina haraka ya kuamua kama itaendelea na Jupp Heynckes kama kocha wake baada ya msimu huu au la. Henyckes mwenye umri wa miaka 67, amepokea sifa nyingi huku Bayern ikiongoza ligi kwa pointi saba na inakaribia kufuzu katika awamu ya maondowano ya mechi za Ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kuizaba Lille magoli sita kwa moja.
Rummenige amesema Jupp amekubali kufanya mazungumzo kuhusu mkataba wake mwaka ujao wa 2013. Heynckes amesema atakaa chini na Rummenige mwezi Machi mwakani ili kuamua kama atasaini upya mkataba wake wa miaka miwili ambao unakamilika mwishoni mwa msimu huu. Rais wa klabu Franz Beckenbauer na kocha wa zamani Ottmar Hitzfeld ni miongoni mwa wanaompigia upatu Heyckes kuongezwa mkataba.
Vita vya kileleni mwa Ligi Uingereza
Tukielekea nchini Uingereza ni kuwa, Baada ya kujikatia tikiti ya awamu ya muondowano katika ligi ya mabingwa, Manchester United inalenga kuendelea faida yake ya nyumbani katika ligi kuu Uingereza wakati itaialika Aston Villa leo Jumamosi.
United ilisonga kileleni mwa ligi kwa kiishinda Arsenal mwishoni mwa wiki iliyopita na huku mahasimu wake wa karibu Chelsea na Manchester City wakijitosa uwanjani kesho Jumapili, ushindi dhidi ya Aston Villa utawaweka vijana hao wa kocha Alex Ferguson kileleni na tofauti ya pointi nne. Baada ya kuichapa Chelsea na Arsenal katika mechi zake mbili za mwisho, United sasa inaanza tena kucheza michuano inayoonekana nyepesi ikiwa ni pamoja na Norwich City kabla ya mechi za nyumbani dhidi ya Queens Park Rangers na West Ham United.
Arsenal ambao walitoka sare ya kufungana mabao mawili kwa mawili na Schalke katika ligi ya mabingwa, wako katika nafasui ya saba, na watawaalika Fulham, ambao na alama sawa na The Gunners. Arsene Wenger atakuwa bila huduma za Jack Wilshere. Everton watacheza leo dhidi ya Sunderland wakiwa katika nafasi ya nne, lakini wnaalenga kumaliza mfululuizo was are mara nne. Jumapili Tottenham itakuwa ugenini dhidi ya Manchester City. Chelsea watakuwa nyumbani kuwaalika Liverpool.
Aliyekuwa mlinda lango wa kimataifa wa Uholanzi Edwin van der Sar anapangiwa kuwa meneja mkurugenzi mpya wa klabu ya Ajax. Taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa mabingwa hao wa Uholanzi imesema kuwa Ajax inafanya magunzumo na van der Sar kuhusu kazi ya usimamizi lakini mazungumzo hayo bado hayajakamilika. Ajax hawajakuwa na meneja mkurugenzi kwa miezi kadhaa baada ya mgogoro kuibuka baina ya Louis van Gaal, ambaye ameondoka na kuteuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi, na kigogo wa Ajax Johan Cruyff.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Abdul-Rahman