1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Afghanistan wafunguliwa rasmi Bonn

5 Desemba 2011

Wajumbe kutoka mataifa na mashirika 100 wanakutana leo hii mjini Bonn, kujadili misaada ya kuipatia Afghanistan baada ya majeshi ya kimataifa kuondoka nchini humo mwaka 2014.

https://p.dw.com/p/13MZd
German Chancellor Angela Merkel gestures during her speech at the German Federal Parliament, Bundestag, in Berlin, Germany, Friday, Dec. 2, 2011. (Foto:Michael Sohn/AP/dapd)
Kansela wa Ujerumani, Angela MerkelPicha: dapd

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ataufungua mkutano huo pamoja na Rais wa Afghanistan Hamid Karzai na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
Miongoni mwa kiasi ya wajumbe 1,000 watakaouhudhuria mkutano huo, ni waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton. Kabla ya mkutano huo, Karzai alisema, Afghanistan hadi mwaka 2024, itahitaji msaada wa kama dola bilioni tano kutoka jumuiya ya kimataifa. Fedha hizo zinahitajiwa kuyajenga majeshi, polisi na taasisi za serikali. Katibu Mkuu Ban pia alisema, utulivu wa kisiasa, unaweza kupatikana nchini Afghanistan baada ya majeshi ya kimataifa kuondoka nchini humo, kama itasaidiwa na majirani wake.