1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa ASEAN waanza mjini Jakarta

5 Septemba 2023

Rais Joko Widodo wa Indonesia leo amewakaribisha viongozi wenzake wa mataifa ya kusini mashariki mwa Asia kwa mkutano wa kilele wa jumuiya ya kanda hiyo, ASEAN, unaofanyika mjini Jakarta.

https://p.dw.com/p/4VySy
Indonesien | Der indonesische Präsident Joko Widodo
Picha: Muchlis Jr/Presidential Secretariat Press Bureau

Mkutano huo unatuama kwa mara nyingine katika kuutafutia ufumbuzi mzozo wa kiasiasa nchini  Mynamar na kushughulikia tofauti zinazojitokeza kwenye kanda hiyo juu ya kutanuka kwa nguvu za China. 

Akizungumzia mivutano iliyo bayana kati ya madola yenye nguvu kwenye kanda hiyo rais Widodo amesema anatambua dunia haiko katika hali nzuri. Amesema changamoto za siku za usoni zitakuwa ngumu zaidi ikiwa ni matokeo ya mapambano ya kuwania ushawishi baina ya nchi zenye nguvu.

Lakini Widodo amesema Jumuiya ya ASEAN imekubaliana kutokuwa uwanja wa vita vya yeyote nawatashirikiana na yeyote kwa ajili ya amani na ustawi.

Ama kuhusu suala la Mynamar mkutano huo wa ASEAN utatathmini utakelezaji wa makubaliano yenye vipengele vitano yaliyofikiwa Aprili mwaka 2021 kati ya kanda hiyo na utawala wa kijeshi wa Mynamar wa kumaliza mzozo unaondelea: