1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa WEF wafunguliwa rasmi huko Davos,Uswisi

21 Januari 2025

Mkutano wa jukwaa la kiuchumi duniani WEF unafunguliwa leo (21.01.2025) katika mji wa kifakhari wa Davos Uswisi na unatarajiwa kugubikwa na agenda kuhusu migogoro mingi mikubwa ya siasa za kikanda.

https://p.dw.com/p/4pQKd
Schweiz Davos 2025 | Impressionen vom Weltwirtschaftsforum
Picha: World Economic Forum Annual Meet/Avalon/IMAGO

Mkutano huo unafanyika siku moja baada ya Donald Trump kuingia madarakani nchini Marekani. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anataka kulitumia jukwaa hilo la kutafuta uungwaji mkono wa nchi yake.

Rais wa Israel Isaack Herzog pia anatarajiwa kuzungumza kwenye jukwaa hili kufuatia kuachiliwa kwa mateka wa nchi hiyo na makubaliano ya kusitisha vita Ukanda wa Gaza.

Davos World Economica Forum

Kansela Olaf Scholz na mwanasiasa anayegombea ukansela kutoka chama cha kihafidhina nchini Ujerumani cha CDU Fredrich Merz pia watazungumza.

Rais mpya wa Marekani Donald Trump pia anatarajiwa kulihutubia jukwaa hilo siku ya Alhamisi.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW