1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Mkutano wa kilele kuhusu Ukraine huko Ramstein waahirishwa

9 Oktoba 2024

Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Ukraine uliopangwa kufanyika katika kambi ya jeshi la Marekani nchini Ujerumani, umeahirishwa baada ya Rais Joe Biden kuahirisha ziara yake kutokana na kimbunga Milton.

https://p.dw.com/p/4laOT
Mkutano wa kilele kuhusu Ukraine huko Ramstein, Ujerumani, waahirishwa
Mkutano wa kilele kuhusu Ukraine huko Ramstein, Ujerumani, waahirishwaPicha: Heiko Becker/REUTERS

Biden alitarajiwa kuwasili Berlin kesho jioni, ambako alipangiwa kukutanana Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz na Rais Frank-Walter Steinmeier.

Baada ya hapo Biden alitarajiwa kuelekea kwenye jimbo la Rhineland-Palatinate kuhudhuria mkutano wa kilele katika kambi hiyo iliyoko Ramstein.

Mkutano huo ulitarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa nchi washirika na wafadhili wakuu wa silaha kwa Ukraine, ambapo ilikuwa wajadiliane kuhusu hatua zaidi ya msaada kwa nchi hiyo katika kujilinda dhidi ya Urusi.

Msemaji wa serikali ya Ujerumani amesema Jumatano (09.10.2024) kuwa bado hakuna tarehe mpya iliyopangwa kwa ajili ya mkutano huo wa kilele.