SiasaLaos
Mkutano wa kilele wa ASEAN wafunguliwa Laos
9 Oktoba 2024Matangazo
Mkutano huo wa mwaka utaangazia jinsi ya kukabiliana na vita vya muda mrefu vya Myanmar, na mivutano kuhusu maeneo katika Bahari ya Kusini mwa China. Mkutano huo pia utagusia kuongezeka kwa ghasia katika eneo la Mashariki ya Kati.
Mkutano huo wa viongozi wa ASEAN, utafuatiwa na mikutano na mataifa yenye nguvu duniani, ikiwemo China, Marekani na Urusi, ambazo zinapigania ushawishi katika eneo hilo. Nchi 10 wanachama wa ASEAN, ni Indonesia, Thailand, Singapore, Ufilipino, Vietnam, Malaysia, Mynmar, Cambodia, Brunei na Laos.
Nchi hizo pia zitafanya mazungumzo na washirika wao Japan, Korea Kusini, India, Australia na New Zealand, kuhusu uchumi, mabadiliko ya tabianchi na nishati.