1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Mkutano wa kilele wa G7 waanza Hiroshima, Japan

19 Mei 2023

Wawakilishi wa mataifa ya kundi la nchi saba tajiri duniani G7, wameanza mkutano wao wa kilele mjini Hiroshima, Japan kwa kuwakumbuka wale waliouwawa kwa bomu la atomiki.

https://p.dw.com/p/4RZLH
Viongozi kwenye mkutano wa kilele wa G7
Viongozi wa kundi la G7 na wawakilishi wa Umoja wa Ulaya wakihudhuria mkutano wa kilele wa kundi hilo mjini Hiroshima.Picha: KYODO via REUTERS

Bomu hilo lililoangushwa mjini Hiroshima na wanajeshi wa Anga wa Marekani mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia, Agosti 6 mwaka 1945.

Viongozi hao walitembelea maeneo ya kumbukumbu ya waathiriwa wa mkasa huo, uliosababisha vifo vya zaidi ya watu 70,000. Bomu lengine liliangiushwa mjini Nagasaki siku tatu baada ya bomu la kwanza kurushwa.

Mkutano huo unaoanza leo hadi siku ya Jumapili utazungumzia kwa upana mgogoro wa Urusi na Ukraine, vikwazo zaidi kwa Urusi na namna ya kukabiliana na uchokozi wa China na madai yake ya kukimiliki kisiwa cha Taiwan.

Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky, anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo. Zelensky amekuwa akiomba kuungwa mkono zaidi na jumuia ya kimataifa katika kile alichokitaja kuwa kujilinda na uvamizi wa Urusi unaonedelea nchini mwake.