1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa jumuia ya nchi za Afrika magharibi-Uma umeakhirishwa kwasababu ya mzozo wa Saharawi

24 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFAm

Tripoli:

Mkutano wa kilele wa nchi za Maghreb-UMA,umeakhirishwa kutokana na mivutano iliyopo kati ya Algeria na Moroko kuhusu Sahara ya magharibi.Duru za kuaminika toka Tripoli zimesema.Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi hizo za Afrika kaskazini wamekua wakikutana tangu jana mjini Tripoli Libya kuandaa mkutano huo wa kilele. Jumamosi iliyopita rais Abdel Aziz Bouteflika wa Algeria alisisitiza juu ya uungaji mkono wa nchi yake kwa madai ya wapigania uhuru wa Saharawi.Matamshi hayo yamekosolewa vikali na Moroko.Waziri wa mambo ya nchi za nje Mohammed Ben Issa amesema matamshi kama hayo hayasaidii kuimarisha shughuli za umma.