Mkutano wa kilele wa mataifa Kinshasa kujadili amani ya DRC
24 Februari 2022Mamilioni ya watu walikufa kutokana na vurugu, magonjwa na kukosa chakula wakati vita mbili za mwaka 1996-7 na 1998-2003 nchini Congo -- mazozo ambao ulizihusisha nchi kutoka Afrika Mashariki na Kati.
Mkutano wa kilele wa Kinshasa, ambao ni wa 10 katika mfululizo huo, umewaleta pamoja marais wa DRC, Afrika Kusini, Uganda, Angola, Jamhuri ya Congo, Burundi na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Mkutano huo wa kilele ulitarajiwa kuelezea wasiwasi kuhusu msaada wa lojistiki na mwingine kwa makundi ya silaha yanayosalia kuwa mashughuli katika eneo hilo.
Pia ulitarajiwa kuzingatia operesheni ya pamoja kati ya DRC na Uganda dhidi ya kundi kubwa la waasi la Allied Demoratic Forces (ADF), alisema mwanadiplomasia moja.
Operesheni hiyo ya kihistoria ilianzishwa katika eneo la mpakani mwishoni mwa Novemba mwaka uliyopita, ikichochewa na mkururo wa mauaji mashariki mwa DRC na mashambulizi ya mabomu katika mji mkuu wa Uganda, Kampala.
Mkutano wa kilele pia utapongeza kuboreshwa kwa uhusiano kati ya Rwanda na Uganda na kati ya rwanda na Burundi, baada ya muda mrefu wa mivutano.
Makubaliano ya 2013 yalisainiwa na jumla ya mataifa 11, zikiwemo Kenya, Sudan Kusini, Tanzania na Zambia. Mkutano ujao wa kilele utaandaliwa na Burundi mnamo mwaka 2023.
Chanzo: AFPE