1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kimataifa juu ya Ukraine wamalizika Jeddah

7 Agosti 2023

Wajumbe kutoka mataifa kadhaa duniani wamekamilisha mazungumzo ya amani kuhusu Ukraine yaliyoitishwa na Saudi Arabia kwa maafikiano ya kuendeleza "mashauriano" ili kujenga msingi wa pamoja wa kupatikana kwa amani.

https://p.dw.com/p/4Uqm8
Saudi Arabien, Dschidda | Ukraine Gipfeltreffen
Picha: Saudi Press Agency/Handout/REUTERS

Maafisa hao wanaojumuisha washauri wa masuala ya usalama na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa walikutana jana kwenye mji wa mwambao wa Jeddah kujaribu kutafuta njia za kumaliza mzozo wa Ukraine.

Kulingana na Shirika la Habari la Saudia (SPA), washiriki wamekubaliana kutumia njia ya mashauriano na kubadilishana mawazo kwa dhumuni la kufikia mwafaka wa njia bora za kuushughulikia mzozo wa Ukraine. 

Soma zaidi: Mazungumzo ya amani kuhusu vita vya Ukraine yafanyika Saudi Arabia

Miongoni mwa mataifa yaliyoshiriki ni Ukraine, Marekani, Ujerumani, China, India, Brazil na Afrika Kusini. Urusi haikualikwa kwenye mazungumzo hayo. 

Mkutano huo umehitimishwa wakati mapambano yanazidi kuwa makali kati ya Urusi na Ukraine, ambapo mwishoni mwa juma pande hizo mbili zimehujumiana kwa kutumia ndege zisizo na rubani.