SiasaKorea Kusini
Mkutano wa Korea-Afrika kuangazia madini na biashara
2 Juni 2024Matangazo
Korea Kusini inauelezea kuwa utalenga kupata uagizaji wa madini muhimu na kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Afrika. Maafisa wa serikali ya mjini Seoul wamesema wajumbe kutoka nchi 48 za Afrika watahudhuria mkutano huo.
Hafla ya marais imepangwa kufanyika Jumanne, na kufuatiwa na mkutano wa kilele wa biashara unaohusisha viongozi wa makampuni ya Korea Kusini na Afrika siku ya Jumatano.
Rais Yoon amesema kuna miradi chungu nzima ambapo Korea na Afrika zinaweza kushirikiana katika nyanja nzima ya miundombinu, ikijumuisha ujenzi wa barabara, reli, viwanja vya ndege na bandari, mifumo mahiri ya jiji, na usafirishaji.