1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa maendeleo ya kiuchumi ya wapalestina waendelea

Oumilkheir Hamidou Zainab Aziz
26 Juni 2019

Maafisa wa nchi za kiarabu,wakuu wa taasisi za kimataifa na wawekezaji wanaendelea kwa siku ya pili na ya mwisho,na mkutano unaosimamiwa na Marekani kuhusu maendeleo ya kiuchumi ya wapalastina

https://p.dw.com/p/3L6o9
Bahrain Eröffnung der "Peace to Prosperity" Konferenz in Manama
Picha: Reuters

Mkutano huo umeanza jana usiku katika mji mkuu wa Bahrain-Manama ikiwa ni sehemu ya juhudi za Marekani za kuufumbua mzozo kati ya Israel na Wapalastina.

"Vitega uchumi katika maeneo ya ukingo wa magharibi na Ukanda wa Gaza vinabidi vilenge katika kubuni nafasi za kazi na miundo mbinu ili kusaidia kuinua shughuli za kiuchumi za Palastina, amesema mwenyekiti wa shirika la fedha la kimataifa IMF Christine Lagarde.

Ukuaji wa kiuchumi unanyweya katika maeneo ya utawala wa ndani wa Palastina ambako nakisi ya haazina ya serikali imefikia asili mia nane.

Indonesien IWF Bali | Lagarde
Mwenyekiti wa Shirika la fedha la kimataifa IMF Christine Lagarde.Picha: Getty Images/AFP/S. Tumbelaka

Idadi ya wasiokuwa na kazi imefikia asili mia 30 katika ukingo wa magharibi wa mtio Jordan na asili mia 50 katika ukanda wa Gaza amesema mwenyekiti wa shirika la fedha la akimataifa IMF, Christine Lagarde kaatika mkutano huo wa Manama.

Jared Kushner, mkwe na mshauri wa rais wa Marekani Donald Trump alisema alipoufungua mkutano huo jana usiku kwamba ukuaji wa kiuchumi kwa wapalastina hautowezekana bila ya "ufumbuzi wa kudumu na wa haki wa mzozo wa kisiasa."

Mpango wa amani utatekelezeka ikiwa matumaini ya amani yatachomoza

Hata hivyo mkutano unalenga fursa za kiuchumi katika juhudi za kutafakari kwa namna mpya kuhusu changamoto hizo" ameongeza kusema. Waziri wa dola wa Saudi Arabia Mohammed al-Sheikh amesema kwa upaande wake mpango wa kiuchumi unaweza kutekelezeka "ikiwa matumaini ya amani yatachomoza kwa watu wote kuweza kushirikiana."

Westjordanland Präsident von Palestina Mahmoud Abbas hält eine Rede zum 12. Todestag  Yasser Arafat
Kiongozi wa Palestina Mahmood Abbas Picha: REUTERS/M. Torokman

Wapalastina wanaususia mkutano huo uliolengwa kukusanya dala bilioni 50 kwaajiöli ya kugharimia miundo mbinu,kuinua shughuli za kilimo na utalii katika maeneo ya utawala wa ndani wa Palastina na pia kugharamia miradi katika nchi jirani za Misri, Jordan na Libnan. Waisrael hawakualikwa.

Wakati huo huo shirika la Umoja wa M ataifa alinalowahudumia wakimbizi wa kipalastina limesema wafadhili wameahidi kuchangia dala milioni 113 kuwasaidia wakimbizi milioni tano wa kipalastina kwa mwaka huu.Shirika la kimataifa la kuqahudumia wakimbizi wa Palastina linasumbuliwa na uhaba wa fedha tangu Marekani ilipoamua kupunguza hadi dala milioni 60 kutokaa msaada wa dala milioni 360 iliyokuwa ikilipatia shirika hilo.

Mwaka huu serikali ya rais Trump haikuchangia hata senti moja.

Vyanzo: dpa/afp/AP