1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa pili baina ya Trump na Kim kufanyika mwezi ujao

Sylvia Mwehozi
19 Januari 2019

Mkutano wa pili wa kilele baina ya rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao.

https://p.dw.com/p/3BpCN
Bildergalerie Kim Trump
Picha: Reuters/The Straits Times/K. Lim

Mkutano wa pili wa kilele baina ya rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao, baada ya kiongozi wa ngazi ya juu kutoka Pyongyang kuitembelea Washington. Msemaji wa Ikulu Sarah Sanders amesema Trump, atakutana na Kim karibu na mwishoni mwa Februari katika eneo ambalo litatangazwa baadae. Sanders amesifu juhudi za Korea Kaskazini za kusaka upatanishi lakini akasema Marekani itaendelea kuiwekea shinikizo taifa hilo sambamba na vikwazo hadi pale itakapoachana na mpango wake wa nyukilia. Kim na Trump walikutana kwa mara ya kwanza mwezi Juni huko Singapore, ambako walitia saini nyaraka ambayo inaitaka Korea Kaskazini kumaliza shughuli za nyuklia katika rasi ya Korea. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mazungumzo ya pili baina ya viongozi hao yanapaswa kutoa ramani ya namna ya kuachana na mpango wa nyuklia na makombora wa Korea Kaskazini.