1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa shirika la biashara duniani Hongkong

13 Desemba 2005

Mazingira yaweza yakawa mhanga katika juhudi za kutaka kurahisisha biashara duniani kwa kuondoa vikwazo.hilo ni onyo la masdhirika ya usafi wa mazingira hata yale ya maendeleo mkutano wa WTO ukianza leo mjini Hongkong.

https://p.dw.com/p/CHLm

Maswali kama ushuru wa forodha,viwango vya kuuza nje nyama,ndizi na nafaka au fidia kwa wakulima kwa kupandisha pamba na kutengeza sukari, mara nyingi huwa usoni katika jukwaa la mazungumzo ya shirika hili.Mara hii mkutanoni,si mazao ya kilimo tu yatakayohanikiza na sio tu kwa kuwa Umoja wa Ulaya unadai biashara ya kilimo irahisishwe mno,bali katika kurahisisha huko, mashirika yameingiwa na wasi wasi.

Bibi Sandra Gallina ni mjumbe wa UU anaehusika na majadiliano ya bidhaa zisizo za kilimo katika shirika la Biashara Duniani (WTO).Katika sekta hii kwenye mazungumzo yanayoendelea sasa ya duru ya maendeleo ya Doha au DDA-Doha Development Agenda,UU unadai kupunguzwa wazi kabisa ushuru unaotozwa chini ya msingi wa mfumo wa Uswisi.

Bibi Sandra anasema,

“Msingi huu una maana ushuru wa juu sana upunguzwe zaidi na sana kuliko ushuru usio wa juu.Kwanini tumechagua mfumo huu ?Kwa sababu jukumu la duru ya mazungumzo ya Doha inalai kupunguzwa kwa ushuru tangu wa juu kabisa hata ule wa usio mkubwa au ufutwe kabisa usiwepo.

Hii ina maana katika duru hii tuna jukumu maalumu.Hii ni duru ambayo tutuwame mno kupunguza ushuru wa juu kabisa na ule mkubwa.”-asema bibi Sandra Gallina.

Umoja wa Ulaya una azma kwa kupunguzwa ushuru huo kufungua milango zaidi kwa vivanda vya Ulaya kuuza bidhaa zao nchi za nje.lakini, katika sekta ya bidhaa zisizo za kilimo,katika shirika hili la biashara mbali na bidhaa za viwandani, bali pia mazao ya misitu na uvuvi.hii ina maana:

Endapo UU ukifaulu katika lengo lake hilo,basi ushuru siku zijazo sio tu utapunguzwa kwa bidhaa za magari,mashini za uchapishaji na Computa,bali pia kwa miti itakayokatwa ovyo-ovyo,samaki au mazao mengine ya baharini.

Bw.Jürgen Kirsch ni mjumbe wa Chama cha ulinzi wa mazingira ‘GREENPEACE’ akihusika na maswali ya biashara na ameingiwa na wasi wasi.Anasema,

“Hatuna kanuni za kimataifa za matumizi bora ya misitu na wala hatuna sheria za kimataifa za uvuvi bora wa samaki bagarini.Ikiwa sasa biashara hii itarahishiwa na kufunguliwa milango wazi,bidhaa zitakua rasisi ,haja itapandaa kwa bidhaa hizo na mahitaji hayo yatabidi yatimizwe.Hali hii italeta dhara kwa bahari ambayo itajionea uvuvi mkubwa kupita kiasi.Na ufyekaji miti misituni halkadhalika utaendelea kutia fora.”-aonya Nw.Jürgen Knirsch wa Greenpeace.

Dharuba gani upunguzaji wa ushuru umedhihirisha,ni mfano wa Brazil:

Baada ya nchi hii ya Amerika Kusini kwa kuruhusiwa ilipe ushuru wa 4% badala ya 12 % kwa samaki wake inaosafirisha katika UU ,Brazil iliweongeza biashara yake mara 6 zaidi kuliko hapo kabla na UU.Ilipanda kutoka Euro milioni 26 hapo 1999 na kufikia Euro milioni 170, 2003.

Lakini sio tu kupunguza ushuru kunazusha wasi wasi.Kuna hofu kwamba mhuri wa usafi wa mazingira wa shirika la Biashara Duniani kama kipingamizi cha biashara huenda ukapandishwa hadhi.

Lakini, kuna mwangaza wa matumaini kwenye mazungumzo haya juu ya mada ya mazingira.kwani, inazungumzwa kupunguza fidia zinazotolewa kwa wavuvi.Endapo wanachama huko Hongkong wakiafikiana kutolipa fidia kwa marekebu zao za uvuvi,hii yaweza ikapunguza hofu ya kuzoa samaki wote bagarini na kuiacha bahari takriban tupu.