1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa ufadhili wa afya wafunguliwa Nairobi

Thelma Mwadzaya26 Juni 2023

Kongamano la kwanza la masuala ya kufadhili miradi na mifumo ya afya linaingia siku yake ya pili Jumanne katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Ni mara ya kwanza kwa Kenya kuandaa kongamano hilo kwa eneo la Afrika Mashariki

https://p.dw.com/p/4T5Bh
Swasiland Aids-Patient bekommt antiretrovirale Medikamente
Picha: picture alliance/dpa

Mkutano huo wa siku tatu unawaleta pamoja wawakilishi kutoka Wizara ya afya, Baraza la Mawaziri, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki, mashirika ya Global Fund, Wakfu wa Gates, USAID na UNAIDS. Kikao kama hiki kiliwahi kufanyika Malawi na Zambia na Kenya ni ya tatu kuwa mwenyeji wa mkutano huo. Kwa upande wake, Umoja wa Afrika, umezipa wajibu wa kuunga mkono mijadala ya njia bora za kufadhili mifumo ya afya ya nchi wanachama. Kwa mujibu wa waziri wa afya wa Kenya Susan Nakhumicha, mijadala kama hiyo inatoa fursa ya kuzungumzia na kusaka njia mujarab za kufadhili mifumo ya afya.

Kwenye kongamano hilo, wataalam wanawasilisha hoja na maelezo ya utafiti kuhusu njia mwafaka za kufadhili mifumo ya afya zitakazowaelimisha watunzi wa sera na kuwawezesha kupambana na changamoto zinazoikabili nchi. Kwa upande wake, serikali ya Kenya inanuwia kujikita kwenye mbinu za kuzuwia magonjwa kwa kufuata kanuni za afya badala ya kusubiria matibabu pale mtu anapougua. Kikao hicho cha kitaifa kinafanyika wakati ambapo sekta ya afya imetengewa shilingi bilioni 141.2 katika bajeti ya mwaka 2023/24. Hiki ni kiwango ambacho kimepungua kwa shilingi bilioni 5.6 kwani bajeti iliyopita sekta ya afya ilitengewa shilingi bilioni 146.8. Anne Waiguru ni mwenyekiti wa baraza la magavana na anaelezea.

Ghana na mapambano dhid ya Malaria

Mkutano huu wa kilele utawapa fursa wadau na baraza la magavana kuwasilisha mapendekezo kadha wa kadha zikiwemo pia njia za kuimarisha utoaji huduma kutoka kwa hazina ya bima ya kitaifa ya afya, NHIF na pia kuzindua mifumo mingine ya ufadhili kwa madaraja tofauti ya vituo vya afya nchini,  zinaeleza duru rasmi.

Hii leo akiwa kwenye hafla nyengine, Rais William Ruto aliwaahidi kuwa madereva wa pikipiki za umma maarufu bodaboda kwamba watajumuishwa kwenye mfumo wa bima ya afya ya taifa, NHIF. Kongamano hilo linakamilika Jumatano hii.