1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uchumi

Mkutano wa wakuu wa fedha waanza nchini India

17 Julai 2023

Mawaziri wa fedha wa G20 na wakuu wa benki kuu za mataifa hayo wameanza mazungumzo kujadili mikataba ya mipangilio mipya ya madeni, mageuzi ya kimataifa ya benki na ufadhili ili kuimarisha uchumi wa dunia unaodorora.

https://p.dw.com/p/4TzTD
Japan | Treffen der G7-Finanzminister | Janet Yellen
Picha: Kazuhiro Nogi/Pool/AP/picture alliance

Waziri wa Fedha wa India Nirmala Sitharaman, ambaye ni mwenyekiti na mwenyeji wa mkutano huo unaofanyika mjini Gandhinagar nchini India, ameanza kwa kuwaambia viongozi hao wa kiuchumikuhusu jukumu walilonalola kuelekeza uchumi wa dunia katika ukuaji imara, endelevu, wenye uwiano na shirikishi.

Soma pia:G20: Nchi maskini duniani kupata afueni ya madeni?

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo akiwa na Waziri wa Fedha wa Marekani, Janet Yellen, Sitharaman amesema kuwa suala kuu katika ajenda za mkutano huo wa siku mbili, litakuwa kuwezesha makubaliano kwa masuala yasiyoweza kutatulika yanayohusiana na kuongezeka kwa madeni.