1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu mpya wa majeshi ya Ukraine ataka mabadiliko

9 Februari 2024

Mkuu mpya wa majeshi ya Ukraine, Oleksander Syrsky, amesema kuwa vikosi vyake vitahitaji kubadilika na kuwa tayari kubadili namna vinavyopambana na vikosi vya Urusi ili kushinda vita.

https://p.dw.com/p/4cEP1
Mkuu mpya wa jeshi la Ukraine, Oleksandr Syrskyj
Mkuu mpya wa jeshi la Ukraine, Oleksandr SyrskyjPicha: Valentyn Ogirenko/REUTERS

Kuteuliwa wiki hii kwa Syrsky mwenye umri wa miaka 59, ndiyo yalikuwa mabadiliko makubwa zaidi katika uongozi wa jeshi la Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi karibu miaka miwili iliyopita.

Soma zaidi: Zelensky anatafakari kumfuta kazi mkuu wa majeshi na viongozi kadhaa

 Syrsky amechukua nafasi hiyo kutoka kwa kamanda mashuhuri Valey Zaluzhny, ambaye Rais Volodymyr Zelensky amemtunuku hadhi ya Shujaa wa Ukraine.

Hata hivyo, msemaji wa ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov, amesema kuteuliwa kwa Syrsky hakutaleta mabadiliko yoyote katika mzozo huo, na kwamba Urusi itaendelea na kampeni yake ya kijeshi hadi malengo yake yatimie.