Umoja wa Mataifa wataka kurejeshwa demokrasia Afrika
12 Septemba 2023Mkuu huyo wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema mwenendo wa kuchukua madaraka kwa nguvu siyo suluhu kwa matatizo yaliyopo.
Katika hotuba yake mbele ya mkutano wa majira ya mapukutiko wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Volker amesema njia pekee kuyashughulikia matatizo ni kuwa na utawa kiraia unaotoa nafasi kwa umma kuwa huru kuikosoa serikali na kushinikiza mageuzi.
Amezungumzia pia athari za mabadiliko ya tabianchi na ukosefu wa huduma muhimu akisema ndiyo yanachangia hali ya kukata tamaa miongoni mwa raia duniani na kuchochea hisia za itikadi kali. Hotuba hiyo ya jumla imemumilika vilevile mizozo ya wakimbizi tangu Myanmar, huko Mexico na hata nchini Mali.
Ukosefu wa usalama nchini Haiti na ukandamizaji wa makundi ya walio wachache ulimwenguni ni sehemu ya masuala mengi yaliyoorodheshwa na mkuu huyo wa haki za binadamu kama changamto zinazoikabili dunia.