1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yatoa tahadhari juu ya athari za Mabadiliko ya Tabianchi

3 Julai 2023

Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk ametahadharisha hii leo kuwa mabadiliko ya tabianchi yanatishia kuleta kipindi kibaya cha njaa na mateso ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/4TLT6
Schweiz | Menschenrechtsrat Volker Tuerk
Picha: Pierre Albouy/KEYSTONE/picture alliance

Turk amewakosoa viongozi wa ulimwengu kwa kuchagua njia za muda mfupi kushughulikia kadhia hiyo. Mkuu huyo wa Haki za Binaadamu ametoa tahadhari hiyo alipokuwa akizungumza kwenye mjadala wa haki ya kupata chakula ulioitishwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva.

Amesema matukio ya hali mbaya ya hewa yamekuwa yakiharibu mazao, mifugo na Ikolojia katika kiwango cha kufanya iwe vigumu kwa jamii za watu duniani kujitegemea tena.

Soma pia: UN:yapitisha azimio muhimukuhusu Tabianchi

Turk amearifu kuwa mwaka 2021 pekee, zaidi ya watu milioni 828 duniani walikabiliwa na baa la njaa huku ikikadiriwa kuwa mabadiliko ya tabia nchi yatasababisha watu wengine milioni 80 kukosa chakula ifikapo katikati mwa karne ya 21.

Amewarai viongozi duniani kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi hivi sasa ili kuepusha janga kwa vizazi vinavyokuja.