Hezbollah yahimiza kuruhusu boti za wahamiaji kuelekea Ulaya
14 Mei 2024Katika hotuba ya televisheni, kiongozi huyo wa Hezbollah ametoa wito kwa mamlaka kufungua njia ya bahari na kuruhusu yeyote anayetaka kwenda Ulaya kwa boti kufanya hivyo.
Hata hivyo, ameeleza kuwa hawalazimishi raia wa Syria waliokimbia makwao kupanda boti na kuelekea Cyprus au nchi nyengine za Ulaya.
Soma pia: Jenerali wa zamani wa Syria kushtakiwa Sweden kwa uhalifu wa kivita
Matamshi yake ameyatoa kama sehemu ya kuushinikiza Umoja wa Ulaya baada ya umoja huo kutangaza mapema mwezi huu msaada wa dola bilioni 1 kwa Lebanon ili kusaidia kukabiliana na wimbi la wahamiaji.
Cyprus, nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya iliyo upande wa mashariki, iko chini ya kilomita 200 kutoka Lebanon na Syria na inataka kuzuia kuondoka kwa boti za wahamiaji kuelekea pwani yake.