Mkuu wa jeshi la polisi Kongo asimamishwa kazi kwa mauaji ya Chebeya
7 Juni 2010Matangazo
Mashirika ya kutetea haki za binaadam katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo yamepongeza hatua ya rais Joseph Kabila ya kumsimamisha kazi inspekta mkuu wa polisi ya nchi hiyo ili kuruhusu uchunguzi wa kifo cha mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu, Floribert Chebeya, aliyeuliwa wiki iliyopita mjini Kinshasa. Hata hivyo, mashirika hayo yameomba uchunguzi zaidi na wa haki ufanyike ili kutathmini sababu za mauaji ya Bwana Chebeya.
Mhariri, Othman Miraji