JamiiUturuki
UN: Awamu ya uokozi yakaribia kumalizika Uturuki, Syria
13 Februari 2023Matangazo
Kulingana na afisa mkuu wa shughuli za kiutu katika Umoja wa Mataifa Martin Griffiths, hatua za dharura zitaelekezwa kwenye utoaji misaada wa chakula, makaazi kwa waathiriwa, shule na ushauri nasaha,
Akiwa mji wa Aleppo nchini Syria , Griffiths amesema Umoja wa Mataifa utahakikisha misaada inapitia maeneo yanayodhibitiwa na serikali hadi kaskazini magharibi yanakodhibitiwa na waasi na ambayo misaada hufika kwa nadra.
Hadi sasa idadi ya vifo imepindukia 35,000. Umoja wa Mataifa umebashiri idadi jumla ya vifo kufuatia janga hilo la tetemeko la ardhi itapindukia 50,000.
Msichana mmoja wa umri mdogo aliyetambuliwa kwa jina Miray ni miongoni mwa manusura wa hivi karibuni zaidi kuokolewa chini ya vifusi.