1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Mkuu wa majeshi Ukraine asema "hali ni mbaya uwanja wa vita"

13 Aprili 2024

Mkuu wa majeshi wa Ukraine, Oleksandr Syrsky, amesema hali kwenye mstari wa mbele wa mapambano mashariki mwa nchi yake imezidi kuwa mbaya katika siku za hivi karibuni kutokana na kupamba moto kwa mashambulizi ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4eigE
Mkuu wa majeshi wa Ukraine, Oleksandr Syrsky,
Mkuu wa majeshi wa Ukraine, Oleksandr Syrsky.Picha: Ukrainian Armed Forces via AFP

Syrsky, aliyeteuliwa mwezi Februari kuchukuwa nafasi ya Valery Zaluzhny, amesema hivi leo kuwa Urusi inaonekana kuwa na silaha za kiwango cha juu.

Mkuu huyo wa majeshi ameonya kwamba  operesheni ya kijeshi ya Moscow imeimarika zaidi tangu ulipomalizika uchaguzi mkuu wa mwezi Machi, ambao ulimrejesha madarakani Rais Vladimir Putin kwa wingi wa kura.

Urusi imerejesha udhibiti wa maeneo iliyokuwa imeyatwaa awali na sasa inasonga mbele kuelekea ndani ya Ukraine. Kyiv inalalamikia kucheleweshwa kwa msaada wa kijeshi wa mataifa ya Magharibi kuwa sababu ya hali hiyo.