1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Modi aikosoa Urusi kwa kushambulia hospitali ya watoto Kiev

9 Julai 2024

Waziri mkuu wa India Naredra Modi amemwambia Rais Vladimir Putin kwamba vifo vya watoto wasiokuwa na hatia katika vita,mgogoro au shambulio la kigaidi ni kitu kinachoumiza sana.

https://p.dw.com/p/4i4Wx
Narendra Modi na Vladimir Putin
Waziri mkuu wa India Narendra Modi na rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Sergei Bobylev, Sputnik, Kremlin Pool Photo/AP/picture alliance

Waziri mkuu wa India Narendra Modi amemwambia Rais Vladimir Putin kwamba vifo vya watoto wasiokuwa na hatia katika vita,mgogoro au shambulio la kigaidi ni kitu kinachoumiza sana.

Kauli ya kiongozi huyo wa India aliyeko ziarani Moscow imekuja siku moja baada ya kushambuliwa kwa hospitali kuu ya watoto mjini Kiev na makombora ya Urusi.Urusi imekanusha kushambulia hospitali ya watoto mjini Kiev.

Waziri Mkuu Modi amemwambia Putin,suluhisho la vita nchini Ukraine haliwezi kupatikana katika uwanja wa vita,bali kupitia mazungumzo ya amani. Hata hivyo Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine, ameikosoa ziara ya Modi akisema imetowa pigo kubwa kwa juhudi za  amani. Amesema inavunja moyo na kusikitisha kuona kiongozi wa nchi kubwa inayojali demokrasia ikimkumbatia muhalifu mkubwa duniani.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW