1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moenchengladbach yaifukuzia Dortmund kileleni mwa Bundesliga

Sekione Kitojo
22 Oktoba 2018

Borussia Moenchengladbach  yaifukuzia Borussia Dortmund sasa kileleni  mwa  Bundesliga, Bayern nayo imo njiani kudai nafasi yake stahili baada ya kupata ushindi wa kwanza baada ya michezo minne.

https://p.dw.com/p/36xto
Deutschland Borussia Mönchengladbach vs 1 FSV Mainz | Jonas Hofmann
Wachezaji wa Borussia Moenchengladbach wakimpongeza mwenzao Jona Hofmann baada ya kufunga bao dhidi ya FSV Mainz Picha: imago/M. Müller

Jonas Hofmann  alipachika  mabao  matatu  jana  ikiwa  ni  mara yake  ya  kwanza  tangu  kuanza  kucheza  kandanda  katika  ngazi ya  juu  jana,  wakati  Borussia  Moenchengladbach  ilipojiweka katika  nafasi  ya  pili  ya  msimamo  wa  ligi  katika  Bundesliga kwa kuizaba  Mainz 04  kwa  mabao 4-0.

Deutschland Borussia Mönchengladbach vs 1 FSV Mainz | Jonas Hofmann
Jonas Hofmann akifurahia moja kati ya mabao yake matatu akiwa na MoenchengladbachPicha: imago/U. Kraft

Baada  ya  ushindi  wa  kushangaza  wa  mabao  3-0  dhidi  ya mabingwa  watetezi  Bayern Munich  wiki  tatu  zilizopita, ushindu huu ni ishara  kubwa  kutoka  kwa  kocha  Dieter Hecking  na  kikosi chake, ambaye  aliiweka  timu  hiyo  katika  nafasi  ya  pili nyuma  ya Borussia  Dortmund ambao  wanashikilia  nafasi  hiyo  baada  ya Jumamosi  kuikandika  VFB Stuttgart  kwa  mabao 4-0  pia.

Ushindi wa  Gladbach umeiacha Bayern Munich  mabingwa  watetezi katika  Bundesliga  katika  nafasi  ya  nne  ikiwa na  pointi 16.

Borussia  Dortmund

Vinara  wa  ligi  hiyo  hivi  sasa  ni  Borussia  Dortmund  ambayo  ina pointi 20, ikifuatiwa  na  Borussia  Moenchengladbach  yenye  pointi 17 sawa  na  Werder  Bremen  timu  ambayo  iliididimiza   makamu bingwa  wa  Bundesliga  Schalke 04 katika  mzozo  mkubwa  baada ya  kuitandika  kwa  mabao 2-0  nyumbani siku  ya  Jumamosi  jioni.

1. Bundesliga VfB Stuttgart - Borussia Dortmund | (0:2) Tor
Marco Reus11, Lukasz Piszczek(kulia) na Paco Alcacer wa Borussia Dortmund wakishangiria baoPicha: picture-alliance/dpa/M. Murat

Schalke 04 iko  nafasi  ya 16  ikiwa  na  pointi 6  tu  kibindoni. Nafasi ya Schalke  kuwania  kucheza  katika  mashindano  ya  Ulaya Champions League ama  Europa  League  imo  mashakani mara  hii, kutokana  na  umbali  uliopo  kati  yake  na  timu  zilizoko  juu.

Bayern Munich  imesafiri  kwenda  Ugiriki  kukabiliana  na  AEK Athens  katika  Champions  League  kesho  Jumatatu ikiimarishwa na  ushindi  katika  Bundesliga  ambao  ni  kama  ukombozi baada ya  kupata  matokeo  mabaya, katika  uchezaji. Mbinyo  ulikuwa ukizidi  kwa  mabingwa  hao  wa Ujerumani  pamoja  na  kocha  wao mpya  Niko  Kovac kutokana  na  kutoshinda  katika  michezo  minne na  kusababisha  viongozi  wa  juu  wa  klabu  hiyo ikiwa  ni  pamoja na  Karl-Heinz Rummenigge  na  Uli Hoeness kushambulia  vyombo vya  habari.

Karl-Heinz Rummenigge
Mwenyekiti wa Bayern Munich Karl-Heinz RummeniggePicha: picture alliance / Matthias Balk/dpa

Lakini  ushindi  wa  mabao 3-1 dhidi  ya  Wolfsburg  katika Bundesliga , ambamo Robert Lewandowski  alipachika  mabao mawili  na  kufikisha  mwisho  ukame  wa  magoli  katika  michezo minne, unasifiwa  kama  sehemu  muhimu  ya  mabadiliko  ya majaaliwa  ya Bayern Munich  msimu  huu.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / rtre / afpe / dpae

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman