1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: AU yataka misaada zaidi

28 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnZ

Umoja wa nchi za Afrika AU unataka misaada zaidi ya kifedha ili kufanikisha mpango wa kuwapeleka wanajeshi zaidi wa kulinda amani wa umoja huo huko nchini Somalia.

Wanajeshi hao wanahitajika kwenda kukisaidia kikosi cha Uganda chenye wanajeshi 1600 ambao wako katika mji mkuu wa Mogadishu.

Wanajeshi hao wamevamiwa na wapiganaji wanaounga mkono mahakma za kiislamu wanaopambana na serikali ya mpito ya rais Abdillahhi Yusuf.

Umoja wa nchi za Afrika unahitaji kikosi cha wanajeshi 8000 watakao hudumu nchini Somalia.