1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Monrovia. Matokeo ya uchaguzi Liberia kutangazwa Jumanne.

13 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEIs

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Liberia imesema kuwa haitatangaza matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais nchini humo hadi ifikapo Jumanne wiki ijayo.

Hii inakuja licha ya kile ambacho kimeonekana kuwa ni ushindi wa wazi wa waziri wa zamani wa fedha Ellen Johnson Sirleaf. Huku asilimia 90 ya kura zikiwa zimekwisha hisabiwa, Sirleaf anaongoza kwa karibu asilimia 60 ya kura.

Mpinzani wake mkuu , mwanasoka mashuhuri George Weah , ametoa shutuma za kufanyika udanganyifu na kutaka uchaguzi huo ufanyike tena . Sirleaf , ambaye atakuwa rais wa kwanza mwanamke kuchaguliwa katika bara la Afrika , ikiwa matokeo yatathibitishwa , amesema kuwa angependa Weah awe katika baraza lake la mawaziri.