1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Monrovia. Raia wa Liberia waanza kuandikishwa kupigwa kura.

26 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFJK

Wananchi nchini Liberia wameanza kujiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa kwanza katika taifa hilo la Afrika magharibi tangu kumalizika kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyochukua muda wa miaka 14.

Uchaguzi huo wa rais wa bunge unatarajiwa kufanyika mwezi wa Oktoba.

Tume ya uchaguzi wa Liberia inatarajia kiasi cha watu milioni 1.5 kiasi cha nusu ya raia wote wa nchi hiyo kujiandikisha kupiga kura.

Hata hivyo kiongozi wa mpito Gyude Bryant ambaye ameiongoza serikali ya mpito tangu pale mapigano yaliyositishwa mwaka 2003, ameeleza kutoridhishwa kwake jana na kujitokeza watu wachache mno hadi sasa wanaojiandikisha.