1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONROVIA: Uchaguzi Liberia, mwanamke kuwa rais Afrika ?

10 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEK1

Katika raundi ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Liberia bibi Ellen Johnson Sirleaf anaongoza kwa asilimia 56 ya kura zilizohesabiwa hadi sasa katika theluthi mbili ya sehemu za kupigia kura.

Mpinzani wake, aliyekuwa mwanasoka maarufu George Weah yupo nyuma , akiwa na asilimia 44 ya kura.Bwana Weah ameilamu tume ya uchaguzi na amedai kwamba udanganyifu umefanyika.Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia amesema kwamba uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.

Iwapo atashinda katika uchaguzi huo,bibi Ellen Johnson Sirleaf atakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa urais barani Afrika.