1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONROVIA:Wapiga kura nchini Liberia,mara ya kwanzya baada ya miaka 14

11 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CESy

Kwa mara ya kwanza baada ya vita vya miaka 14 watu nchini Liberia leo wanapiga kura kumchagua rais .Wastahiki wapatao milioni moja na nusu pia watawachagua wabunge.

Miongoni mwa wagombea wadhifa wa urais ni aliyekuwa mcheza kandanda wa kimataifa George Weah.

Liberia ilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika rasmi mwaka juzi baada ya kiongozi wa wakati huo bwana Charles Taylor kukubali kuenda kuishi katika hifadhi ya kisiasa nchini Nigeria.Askari alfu 15 wa Umoja wa Mataifa wapo nchini Liberia kulinda amani.

Wadadisi wa siasa wanasema bwana George Weah ana matumaini mazuri katika uchaguzi wa leo.Hatahivyo wapo wagombea wengine 20 wenye uzoefu mkubwa wa kisiasa.