1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONUSCO walaani mashambulizi ya M23

27 Januari 2023

Kikosi cha Umoja wa Mataifa kinacholinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) kimelaani mashambulizi ya waasi wa M23 mashariki mwa nchi hiyo ambayo yamewafanya mamia ya watu kuomba hifadhi kwa MONUSCO.

https://p.dw.com/p/4MmPA
Demokratische Republik Kongo | Soldaten am Flughafen in Goma
Picha: Alain Uaykani/Xinhua/IMAGO

MONUSCO iliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba M23 wanapaswa kusitisha uhasama na waondoke kwenye maeneo inayoyakalia, kulingana na mpango wa amani uliowekwa katika mkutano mdogo wa Luanda.

Lakini ripoti ya ndani ya Umoja wa Mataifa inasema waasi hao wamekuwa wakiupuuza mpango wa kusitisha mapigano na kujiondoa.

Soma zaidi: M23 wazidi kuteka maeneo mashariki ya Kongo

Rwanda yasema ndege ya kivita ya Kongo ilikiuka anga yake

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, alisema watu waliokimbia mapigano wamepatiwa mahema, chakula, maji na huduma ya kwanza.

Mashahidi wawili waliokimbia Kitshanga walisema waasi wamechukua udhibiti wa mji huo.

Mwandishi habari aliyeko Kitshanga ambaye aliomba kutotajwa jina kwa sababu za kiusalama, amesema wanajeshi wameondoka kwenye eneo hilo.