1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Morocco kujenga upya nyumba zilizoporomoshwa na tetemeko

Sylvia Mwehozi
15 Septemba 2023

Morocco imetangaza kuzindua mpango wa ujenzi mpya wa nyumba za makaazi takribani 50,000 zilizoporomosha na tetemeko baya la ardhi la wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/4WMUW
Marokko Tafeghaghte | Schweres Erdbeben | Rettungseinsätze
Picha: Fadel Senna/AFP/Getty Images

Morocco imetangaza kuzindua mpango wa ujenzi mpya wa nyumba za makaazi takribani 50,000 zilizoporomosha na tetemeko baya la ardhi la wiki iliyopita.

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 6.8 katika kipimo cha Richter kuwahi kutokea nchini Morocco, limewaua watu karibu 3,000na kuwajeurhi zaidi ya 5,000 kusini mwa mji ulio kitovu cha utalii wa Marrakesh.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Kifalme imesema kuwa watu wote walioathirika watapewa makaazi ya muda katika maeneo yaliyotengwa kustahimili hali ya hewa ya baridi. Mamlaka za Morocco pia zimeagiza msaada wa haraka wa dirham 30,000 elfu sawa na karibu dola 3,000 kwa kaya zilizoathiriwa na maafa.

Idadi rasmi ya watu walioachwa bila makaazi na tetemeko hilo, ambalo limeharibu vijiji vingi katika eneo la milima la Atlas nchini Morocco, bado haijulikani.