Morocco mwenyeji mkutano wa AU
16 Novemba 2016Matangazo
Takribani viongozi 30 wakuu wa Kiafrika wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo wa kilele, akiwemo Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Muhammadu Buhari wa Nigeria.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir, ambaye anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) pia anahudhuria mkutano huo.
Mkutano huo unafanyika pembezoni mwa mkutano wa kimataifa wa kujadili mabadiliko ya tabia nchi unaoandaliwa na Umoja wa Mataifa mjini Marrakesh.
Rais Francois Hollande wa Ufaransa anatarajiwa kuwahutubia viongozi hao wa Afrika.
"Mkutano huu ni fursa kwa viongozii wa Afrika kuratibu misimamo yao na kuzungumza kwa kauli moja ili kujilinda", alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco, Salaheddine Mezouar.