1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MORONI : Umoja wa Afrika wazima mivutano Comoro

7 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFFw

Wawakilishi wa Umoja wa Afrika wakiongozwa na Afrika Kusini jana wamekuwa katika harakati za kuzima kuzuka kwa mvutano visiwani Comoro kwa kuhofia mizozo mipya kati ya viongozi wa visiwa hivyo inaweza kuvuruga makubaliano ya kukomesha miaka 30 ya ukosefu wa utengamano visiwani humo.

Wanasiasa wanaopingana walikubaliana kuhsirikiana madaraka kulikojumuishwa kwenye katiba hapo mwaka 2001 kwa lengo la kukomesha mkondo wa mapinduzi na mfarakano baina ya visiwa lakini mizozo juu ya utekelezaji imepamba moto katika wiki za hivi karibuni.

Serikali ya Rais Assoumani Azaly iliyoko katika kisiwa cha Grande Comoro ilishambulina kwa kukiuka makubaliano hayo na viongozi wa visiwa vya Moheli na Anjouan vyenye mamlaka fulani ya kujiamulia mambo yao baada kuzuwiya uteuzi wa viongozi wa kampuni ya simu ya taifa.