MOSCOW: Chama cha Kijani chakatazwa kugombea uchaguzi
28 Oktoba 2007Matangazo
Tume kuu ya uchaguzi nchini Urusi imekataa ombi la chama cha Kijani kutaka kushiriki kwenye uchaguzi wa bunge.
Vyombo vya habari nchini Urusi vimeripoti kwamba chama cha Kijani ni chama cha kwanza kunyimwa nafasi ya kushiriki katika uchaguzi huo.
Tume ya uchaguzi ya Urusi imekataa maelfu ya saini kwenye stakabadhi zilizowasilishwa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.
Vyama 11 vimesajiliwa kushiriki kwenye uchaguzi huo wa bunge nchini Urusi.