1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow yaonya nchi za Magharibi kuhusu maafisa wake

29 Novemba 2023

Urusi imesema nchi za Magharibi zilijaribu kuwazuia maafisa wake kuhudhuria mkutano wa kila mwaka wa mawaziri wa shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya - OSCE.

https://p.dw.com/p/4ZazC
Moscow | Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria Zakharova
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria ZakharovaPicha: Valery Sharifulin/TASS/dpa/picture alliance

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov, anayekabiliwa na vikwazo vya Ulaya, alilazimika kuombaruhusa ya kurukakatika anga ya Umoja wa Ulaya ili kuhudhuria mkutano huo wa siku mbili, ambao umeanza leo katika mji mkuu wa Macedonia ya Kaskazini, Skopje.

Soma pia:Mwanadiplomasia mkuu wa Latvia ataka nafasi ya juu NATO, akiahidi maono ya wazi kuhusu Urusi

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria Zakharova amesema kuna juhudi za baadhi ya nchi za Magharibi kufanya kila liwezekanalo kuzuia ushiriki wa kawaida wa Urusi katika mkutano huo wa usalama.

Ukraine na mataifa ya eneo la Baltiki wamesema watasusia mkutano huo kama Lavrov atahudhuria, wakihoji kuwa Urusi inapaswa kutengwa kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema atahudhuria mkutano huo wa Skopje, lakini hatokutana moja kwa moja na Lavrov.