1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mripuko wa bomu Pakistan waua watu 91.

28 Oktoba 2009

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton amesema Marekani inaunga mkono operesheni ya jeshi la Pakistan dhidi ya wapiganaji wa Kitaliban huko kusini mwa Waziristan.

https://p.dw.com/p/KHi2
Eneo la mripuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari, mjini Peshawar, Pakistan.Picha: AP
South_Africa_US_Africa_Clinton_XKP108_522243107082009.jpg
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton katika ziara yake ya kwanza Pakistan.Picha: AP

Clinton ambaye yupo katika ziara yake ya kwanza nchini Pakistan kama Mwanadiplomasia mkuu wa Marekani, alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya mripuko mkubwa wa bomu kutokea katika mji wa Peshawar. Watu 91 waliuawa, wengi wao wakiwa ni wanawake.

Ilikuwa ni kama tetemeko kubwa la ardhi, huku waathiriwa wengi wakishindwa kuhimili moto mkubwa uliotokea. Hivi ndivyo baadhi ya walioshuhudia mripuko huo wa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari huko Peshawar walinukuliwa wakisema- huku operesheni za uoakoaji zikiendelea.

Waokoaji wamekuwa wakijishughulisha na kuinua vifusi vya majengo yaliyoporomoka ili kutafuta manusura- Wengi waliokufa wanasemekana ilikuwa ni wanawake. Maduka na biashara zilikatizwa katika eneo hilo la mkasa ambalo ni mashuhuri kwa biashara za bangili, nguo pamoja na vikaragosi vya watoto. Hospitali za Peshawar, ndio majonzi yalijaa zaidi, huku manusura wakijaribu kutafakari uzito wa kuwapoteza wapendwa wao. Na huku Pakistan ikiendelea kukumbwa na misururu ya mashambulizi kufuatia operesheni yao dhidi ya wataliban, mshirika wao mkuu Marekani wamesema watasimama imara na taifa na watu wa Pakistan kuangamiza maadui wa Pakistan.

Flash-Galerie Pakistan: Opfer von Selbstmordanschlag in Lahore, Pakistan
Majeruhi katika hospitali za Peshawar kufuatia mripuko huo wa bomu.Picha: AP

Ujumbe huu ulitolewa na Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton ambaye yupo katika ziara yake ya kwanza nchini Pakistan.

Mwenzake wa Pakistan Shah Mehmoud Qureysh alisema shambulizi la leo na mashambulizi mengine nchini Pakistan hayatalemaza ari ya serikali ya kukabiliana ipasavyo na wapiganaji wa Kitaliban. Tutawasaka, tutawamaliza, kwa sababu nia yetu ni kuwalinda wananchi wa Pakistan aliongeza Qureysh.

Clinton pia alitumia ziara hii yake nchini Pakistan kuzindua mpango wa Marekani unaotoa usaidizi kwa Pakistan kusaidia katika kusambaza nguvu za umeme. Mpango huo mpya ni wa kiasi cha dola milioni 125. Pakistan inakabiliwa na changamoto kubwa ya ugavi wa nishati ya umeme. Kwa sasa serikali ina uwezo tu wa kutoa aslia mia 80 ya umeme kwa matumizi ya raia wake. Hivyo wakati mwingi maeneo mengi nchini Pakistan yanakuwa hayana umeme, ilhali Viwanda vingi nchini humo vinaathirika kutokana na uhaba wa nishati ya umeme ya kuendesha shughuli zao.

Mwandishi: Munira Muhammad/ AFPE

Mhariri: Abdul-Rahman.