AfyaJamhuri ya Kongo
Mripuko wa Mpox umeshaua watu 1,100 kote Afrika: CDC
17 Oktoba 2024Matangazo
Hayo yamesemwa na mkuu wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa barani Afrika CDC, Jean Kaseya mnamo siku ya Alhamisi.
Idadi kubwa ya vifo vimetokea katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambayo ndiyo kitovu cha mripuko wa homa hiyo.
Kaseya ametahadharisha kwamba maradhi hayo yanapindukia kiwango cha kuweza kudhibitiwa bila hatua yoyote kuchukuliwa.
Kaseya ameongeza kwamba kila wiki, bado kuna visa zaidi vya homa ya mpox vinavyoandikishwa kila wiki.
Mkuu huyo wa Afrika CDC amesema kwamba jumla ya visa 42,000 vimesajiliwa barani Afrika tangu mwezi Januari huku Zambia na Zimbabwe zikiripoti kuandikisha visa kwa mara ya kwanza.