1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msafara wa ubalozi wa Marekani washambuliwa Nigeria

17 Mei 2023

Polisi ya Nigeria inasema watu waliojihami kwa bunduki wameushambulia msafara wa wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani kaskazini mashariki mwa Nigeria, ambapo watu wawili pamoja na polisi wameuwawa.

https://p.dw.com/p/4RUjR
Nigeria | Verleihung der Nationalen Ehrenauszeichnung
Picha: Ubale Musa/DW

Wavamizi hao waliufyatulia risasi msafara huo katika barabara moja kuu huko Ogbaru katika jimbo la Anambra ambalo kulingana na polisi, ni kitovu cha machafuko ya wanaotaka kujitenga kutoka Nigeria katika eneo hilo.

Kikosi cha pamoja cha maafisa wa usalama kilifika katika eneo hilo ila kilikuwa kimechelewa kwani wavamizi hao walikuwa wameshatoweka na kuwateka nyara maafisa wawili wa polisi na mmoja wa madereva.

Hakuna raia yeyote wa Marekani aliyekuwa katika msafara huo ulioshambuliwa.