Msalaba Mwekundu waonya mzozo wa kiafya nchini Syria.
16 Februari 2023Matangazo
Katibu mkuu wa shirikisho la kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilal Nyekundu Jagan Chapagain amesema familia zinazokaa kwenye makazi ya muda kwa muda mrefuzinahitaji umeme kwa ajili ya kupasha joto makazi hayo, ambayo ni pamoja na vyumba vya madarasa, ili kuepusha uwezekano mkubwa wa kuugua.
Soma pia:Manusura bado wanaendelea kupatikana kufuatia tetemeko Uturuki na Syria
Amesema hayo baada ya kurejea kutoka Aleppo nchini Syria ambako kwa miaka kadhaa kumeshuhudiwa mapigano makali ya wenyewe kwa wenyewe. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR linakadiria watu milioni 5.3 huenda watakosa makazi kutokana na tetemeko hilo, iwapo hawatasaidiwa.