1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshikamano na George Floyd katika Bundesliga

1 Juni 2020

Baadhi ya wachezaji katika walionekana kuonyesha uungaji mkono wa haki kupatikana kwa Mmarekani mweusi aliyeuwawa na polisi George Floyd jambo lililochochea maandamano si Marekani tu bali katika nchi zengine pia.

https://p.dw.com/p/3d71w
Deutschland Bundesliga - SC Paderborn v Borussia Dortmund | Jadon Sancho 'Justice for George Floyd'
Picha: Reuters/L. Baron

Jadon Sancho baada ya kufunga goli, alivua fulana yake na kuonyesha ujumbe aliokuwa ameuandika ukisema "haki kwa George Floyd". Mchezaji mwenzake hapo dortmund Achraf Hakimi pia alikuwa na ujumbe sawa na huo.

Deutschland Paderborn | Bundesliga | Achraf Hakimi Mouh
Achraf Hakimi akiwa na ujumbe kama wa SanchoPicha: Getty Images/L. Baron

Katika mechi ya Borussia Moenchengladbach na Union Berlin ambapo Gladbach waliebuka kidedea nne moja, mshambuliaji Marcus Thuram baada ya kufunga goli alionekana akipiga goti kama ishara ya kuonyesha mshikamano na George Floyd ambaye alifariki baada ya kuwekewa goti shingoni na afisa wa polisi.

Borussia Mönchengladbach  1. FC Union Berlin Marcus Thuram
Marcus Thuram mshambuliaji wa Borussia MönchengladbachPicha: picture-alliance/dpa/M. Meissner

Katika mpambano ule wa Schalke na Werder Bremen, mchezaji wa Schalke ambaye ni raia wa Marekani Weston McKennie alivaa utepe uliokuwa na ujumbe kama ule aliokuwa nao Sancho kwenye fulana yake akitaka haki kwa George Floyd.